KCB Bank, kupitia dirisha la huduma zinazofuata Misingi ya Sharia, Sahl Banking, lina lengo la kutoa suluhisho za kibenki zinazohamasisha ushirikishwaji wa kifedha lakini pia zikichangia ajenda yetu ya uendelevu (sustainability).
Kupitia huduma hizi, tunatoa nafasi ya ushiriki wa kifedha kwa watu wote bila kujali imani, kwa misingi ya uwazi na maadili. Huduma za Sahl Banking si kwa Waislamu pekee bali zinapatikana kwa yeyote anayehitaji huduma za kifedha zinazofuata Misingi ya Shariah.
Kwa bidhaa kama Sahl Cub Account, Sahl Simba Savers Account, na Hajj Account, tunawawezesha wateja wetu kuweka akiba na kuwekeza kwa njia inayofanana na maadili yao. Shabaha yetu sio tu kusaidia ukuaji wa kiuchumi bali pia inakuza ustahimilivu na usawa wa kijamii, ikileta matokeo chanya katika mazingira na maisha ya wateja wetu.
Akaunti zinazozingatia Shariah
KCB Sahl Banking inatoa akaunti mbalimbali za akiba za Kiislamu zilizoandaliwa ili kukuza ushirikishwaji wa kifedha huku zikiheshimu maadili ya kibenki:
Sahl Cub Account: Imetengenezwa mahsusi kwa wazazi kuweka akiba kwa ajili ya watoto wao, ikihakikisha kuwa na fedha za elimu na mahitaji muhimu zinapatikana bila changamoto.
Sahl Simba Savers Account: Akaunti ya akiba ambayo inawawezesha watu binafsi kuweka akiba bila kupata riba, inayofaa kwa usimamizi wa kifedha wenye uwajibikaji.
Sahl Salary Account: Inarahisisha usimamizi wa mishahara bila wasiwasi wa riba, ikirahisisha utunzwaji wa mishahara pamoja au posho.
Hajj Account: Inawasaidia watu kuweka akiba maalum kwa ajili ya ibada ya Hijja ikiwaruhusu kutimiza wajibu wa kiimani kwa urahisi.
KCB Bank inasisitiza kuwa bidhaa zake zinazozingatia Shariah zinapatikana kwa watu wote, iwe ni watu binafsi au mashirika yanayohitaji huduma za kibenki zisizo na riba. Ushirikishwaji huu unakuza ushirikiano wa jamii na unaruhusu kila mwanajamii kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
KCB Bank Tanzania inahakikisha kuwa bidhaa zake zinazofuata Shariah zinapatikana kwa watu wote zikiwemo taasisi na mashirika mbalimbali, ikichochea ushirikishwaji wa jamii na kuwezesha kila mmoja kushiriki katika shughuli za kiuchumi. Kwa kutoa fursa ya kupata bidhaa hizi, tunahamasisha uwekezaji katika elimu, ukuaji wa biashara, umiliki wa nyumba, na maendeleo ya binafsi.